Nyumbani Forum Ingia
Forum / Bus Simulator Tanzania

Tusaidie kuboresha Bus Simulator Tanzania

Matheo 18 siku iliyopita 28 views 1 majibu
10 Jul 2026 02:30 #1
**Tusaidie kuboresha Bus Simulator Tanzania**

Kama umecheza Bus Simulator Tanzania na umeona changamoto yoyote, tafadhali ripoti hapa forum ili tuweze kuifanyia kazi.

Unaweza kuripoti mambo kama:

* Game kustuck au kuwa nzito kwenye simu yako
* Controls kufanya kazi tofauti na ulivyotarajia
* Steering wheel kuzunguka vibaya
* Basi kutokujibu vizuri kwenye acceleration au brake
* Abiria kutopanda au kushuka vizuri
* Milango kutofunguka au kufungwa vizuri
* Route au kituo kuwa na tatizo
* Graphics kuwa nzito kwenye simu yako
* Malipo/activation/account kuwa na changamoto
* Bug yoyote uliyoiona wakati wa gameplay

Unaporipoti bug, tafadhali andika:

1. Simu unayotumia
2. Version ya Android
3. Sehemu bug ilipotokea
4. Ulikuwa unafanya nini kabla ya bug kutokea
5. Screenshot au video kama inawezekana

Maoni yako yatatusaidia kuifanya Bus Simulator Tanzania iwe bora zaidi kwa wachezaji wote.
27 Jul 2026 19:37 #2
Lina ganda ganda na watu hawaonekani

Ingia ili uweze kujibu mada hii

Ingia Jisajili Bure